ELIMU SAHIHI YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KWA WATOTO

0

Jamii imetakiwa kuhakikisha inawajengea uwezo watoto kwa kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na ujasiriamali itakayoweza kuwasaidia kuwa wabunifu katika stadi mbalimbali ambazo zitawawezesha kujitegemea na baada ya kuhitimu waweze kujiajiri.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Dailey innocent Mwalimu Mkuu Shule ya DCT BISHOP STANWAY wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanafunzi kutambua madhara ya mitandao ya kijami na kuwajengea uwezo wa uninitiated na stadium za kazi

Amebainisha kuwa Ni muhimu wanafunzi hao kupatiwa mafunzo hayo ili baada ya wanafunzi kuhitimu elimu yao msingi na sekondari itawasaidia ili kuondokakana na utegemezi wa ajira kutoka
Serikalini hasa katika wakati huu wa wimbi kubwa la wasomi.

“Samaki mkunje angali mbichi, usemi huo unatafsiriwa vyema kwa vitendo katika kumtayarisha mtoto kimaisha,”anasema

Nao baadhi ya Wanafunzi wa mafunzo hayo, wamesema mafunzo hayo yanakuja na faida nyingi ikiwemo kuwapatia ujuzi watakao utumia mara baada ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi.

Akizungumza kwaniaba ya wanafunzi hao,Rayvan Miyambo amesema mafunzo hayo ni muafaka kwao nakushukuru kwa mafunzo hayo ambayo yatawajenga.

Kwa upande wao wazazi nao hawakuwa nyuma kuelezea umuhimu wa mafunzo yatolewayo kwa watoto shuleni hapo ampo wameeleza ni kwa namna gani mafunzo hayo yanafaida kwa kizazi cha sasa na Baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *