NAIBU WAZIRI SILLO ALITAKA JESHI LA POLISI KUZINGATIA HAKI NA WELEDI

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb) amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia haki, weledi na uadilifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Mhe. Sillo amesema hayo wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma na kuzungumza na Makamisha na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Aprili 4,2024.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeendelea kutekeleza makujukumu yake kwa weledi na uadilifu katika kuhakikisha shughuli za kila siku za Jeshi hilo zinaendelea kufanyika kwa kutoa huduma bora na zenye viwango kwa Wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *