BAJETI YA WIZARA YA KILIMO 2024/25 YAPITISHWA KWA KISHINDO BUNGENI
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeidhinisha matumizi ya ya Shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya Wizara ya Kilimo katika mwaka 2024/2025 kwa ajili ya utekelezaji wa mipango mbalimbali iliyoainishwa ili kuendelea kukuza Sekta ya Kilimo nchini.
Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) amesema Wizara imeongeza kipaumbele kimoja na hivyo kufanya vipaumbele vya mwaka 2024/2025 kuwa sita (6) vitakavyotekelezwa kupitia mikakati 27.
Vipumbele hivyo ni pamoja na kuongeza tija na uzalishaji (Increase Productivity and Production), kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo,kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi, kuimarisha Maendeleo ya Ushirika pamoja na kuimarisha Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA katika Uendelezaji wa Sekta ya Kilimo.