SERIKALI YATOA MIL. 800 UJENZI SOKO LA SAMAKI LUDEWA

0

Serikali Imeoa fedha kiasi cha Sh. Mil. 800 kwaajili ya ujenzi wa soko la samaki katika kata ya Manda Wilayani Ludewa mkoani Njombe litakalo wezesha wavuvi wa ziwa Nyasa na wafanyabiashara wanaouza samaki kufabya biashara pasipo wasiwasi wa kuharibikiwa.

Akizungumza katia mkutano wa utambulishwaji wa mradi Mtaalamu kutoka Idara ya Miundombinu Michael Mbyalo amesema ujenzi wa soko hilo tayari mchakato wake umekwisha anza ambapo kuanzia sasa Mkandarasi ataleta vifaa na ndani ya wiki mbili zijazo ujenzi utaanza na unatarajiwa kukamilika Desemba 14 mwaka huu.

Aidha kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Sunday Deogratius amesema soko hilo limekuja katika muda muafaka kwani kwa sasa wanatarajia kuanza kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali ili viweze kuweka vizimba na kufanya ufugaji wa samaki katika vizimba hivyo.

“Tayari tulishafanya majatibio ya ufugaji wa vizimba na ukawa na matokeo mazuri hivyo kwa sasa tunaka wavuvi wetu wajikite katika ufugaji wa vizimba ili watakapokosa samaki katika uvuvi wa kawaida soko lisikaukiwe na samaki kwakuwa watavuliwa katika vizimba”, Amesema Deogratius.

Josaya Luoga ni Katibu siasa na Uenezi mkoa wa Njombe amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa mradi huo unajengwa kwa viwango vinavyo hitajika na umalizike kwa wakati huku Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani humo Stanley Kolimba akisema chama hicho ndicho chama chenye kujali wananchi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *