ANASWA KWA KUJIFANYA MWANDISHI WA HABARI

0

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mtu mmoja aitwae Rafael Mrutu mkazi wa Same akiwa anafanya shughuli ya maudhui ya Kimtandao bila leseni.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika mtuhumiwa huyo anamiliki on line tv iitwayo Ebenezer 24 TV ambayo haijasajiliwa kisheria ambapo alikamatwa baada ya kurusha maudhui ya ki uchochezi dhidi ya Serikali na Chama cha Mapinduzi na Wananchi wa kijiji cha Bangalala.

Alisema kuwa, mtuhumiwa huyo aliyachukua maudhui hayo kwenye kikao cha wananchi wa kijiji hicho majira ya saa kumi jioni walipokuwa wanaelezea kero ya Ardhi Yao kuchukuliwa na wawekezaji pasipo ridhaa yao.

Inadaiwa kuwa, mtuhumiwa huyo aliitwa na baadhi ya Viongozi ambapo walimlipa kiasi cha fedha ili kuhakikisha habari hizo zinaruka.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuwa wanaendelea na uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyo

imeandaliwa na Na Ashrack Miraji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *