KITUO CHA UMEME DEGE CHALETA NEEMA KWA WANANCHI

0

Menejimenti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke wameungana na Watumishi wa Kituo Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Dege kuadhimisha miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake kwani kimekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na maeneo jirani katika kutoa huduma bora ya umeme.

Akizungumza leo Aprili 30, 2024 Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kusherekea Maadhimisho ya miaka mitatu ya Kituo Cha kupokea na Kupoza umeme Cha Dege yaliyofanyika katika ofisi ya Kituo hicho, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke Mhandisi Ezekiel Mashola, amesema kuwa kituo cha Dege kimekuwa na mafanikio makubwa ya kutatua changamoto ya umeme katika Wilaya ya Kigamboni.

Mhandisi Mashola amesema kuwa Serikali kupitia TANESCO walifanikiwa kujenga Kituo hicho kwa gharama ya shilingi bilioni 26 ili kuhakikisha wakazi ya Wilaya ya Kigamboni wanapate huduma bora ya umeme.

“Tunampango wa kujenga Kituo Kituo kingine cha kupoza umeme kisarawe II ambacho kitakuwa maalamu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wa viwanda” amesema Mhandisi Mashola.

Mhandisi Ezekiel Mashola amempongeza msimamizi wa Kituo cha kupokea na kupoza cha Dege Nurdin Mally kwa jitihadi kubwa anazofanya katika utendaji wa kazi.

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Kigamboni Ramadhani Bilali, amesema kuwa kabla ya Kituo cha Dege kujengwa walikuwa wanategemea miundombinu ya umeme kutoka Kituo Cha kurasini ambapo matumizi ya umeme kwa wakati huo yalikuwa megawatt 18.

Amesema kuwa kwa sasa matumizi ya umeme katika Wilaya ya Kigamboni ni megawatt 46, huku akifafanua kuwa kituo kimechangia kuleta ongezeko la wateja ya huduma ya umeme kwa kiasi kikubwa na kuongeza mapato ya Shirika.

Nae Msimamizi wa Kituo cha kupokea na kupoza umeme Cha Dege Mhandisi Nurdin Mally, amesema kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa mradi mpya katika kituo hicho na baada ya kukamilika mradi huo watakuwa na megawatt 180.

Nae Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa wa Dege, Ramadhani Tumbo ameishukuru TANESCO kwa kuwapatia wananchi huduma ya umeme ya uhakika ambayo haina usumbufu wa kukatika.

“Miaka ya nyuma umeme ulikuwa hauna nguvu na unakatika kila wakati, lakini sasa imekuwa fursa kwetu kwani viwanda vimeongezeka kutokana na uwepo wa umeme wa uhakika” amesema Tumbo.

Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Dege kimekuwa mkombozi wa kukuza shughuli za kiuchumi na kijamii katika Wilaya ya Kigamboni na maeneo jirani kutokana na kuimarisha upatikanaji wa umeme tangu kianze kufanya kazi mwaka 2021.

Maeneo ya Viwandani, Pemba Mnazi, Mwasonga, Mwongozo, Kimbiji na maeneo jirani awali yalikuwa yanapata changamoto ya umeme kukatika au kuwa mdogo kutokana na njia ya umeme kusafiri umbali mrefu kutokea Mkoa wa Kitanesco wa Ilala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *