UZINZI CHANZO CHA VIJANA KUSHINDWA KUFIKIA MAFANIKIO

0

Imeelezwa kuwa Changamoto za kimahusiano zimekuwa zikiwapelekea Vijana na Mabinti kushindwa kutimiza malengo yao na ndoto zao kwa kuchukua maamuzi mbalimbali ikiwemo kukata tamaa ya maisha.Pia zipo changamoto ambazo zimetajwa kuwa ndo sababu ya Vijana kukosa maadili, hofu ya mungu, Elimu na hata kuharibikiwa ndio maana Leo hii tunaona kundi kubwa la vijana limejikita katika matumizi mabaya ya mtandao na kuona wakitukana Viongozi wa Serikali.

Kutokana na hilo imeonekana ipo haja ya kufanya Makongamano pamoja na Semina mbalimbali ili kuwanusuru Vijana.
Kwa moyo wake, wito wake kutoka kwa mungu Mwalimu Joyce Kisha, ambaye ni Mwalimu wa Neno la Mungu kwenye eneo la Vijana ambaye amekuwa akitoa huduma iitwayo Daughter's and Son's of Jerusalem katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwaelimisha vijana na kujifanya kujitambua na kuwasaidia kwenye changamoto walizonazo.

Licha ya kutoa huduma katika mitandao ya kijamii Mwalimu Joyce Kisha ameona kuna haja ya kufanya makongamano na Semin a kwa vijana ili kuwapa Elimu hiyo.na kwa mara ya kwanza Amefanya kongamano Jijini Dodoma ambalo limefanyika katika ukumbi wa Veta leo 27 April, 2024 likiwakutanisha Vijana kutoka Vyuo mbalimbali.

Watoaji Elimu wengine waliokuwepo katika Kongamano hilo ni Wataalamu wa Saikolojia, Afya ya Akili nakadhalika.

Akielezea kuhusiana na Huduma hiyo Mwalimu Joyce anasema amegundua kuwa Vijana wamekuwa wakifanya mahusiano ya ndoa kabla ya ndoa ambapo ameandaa Kitabu kinachoitwa “Principle of Love for Marriage” kinachofundisha kuhusu Ndoa na ukweli wa mahusiano kuweza kutambua mpenzi yupi sahihi kwako, wakati gani unatakiwa kumpenda Mtu, na kuepuka kudanganywa. Kitabu kingine ni “Nguzo Nne kwa kijana” ambapo kijana atajifunza namna anavyopaswa kuwa na yapi ya kuzingatia kwake ili kuvuka Salama na kumsaidia kufanikiwa.

Amesema kupitia huduma hiyo anatarajia kujenga familia zilizo bora kwa kuwapa Elimu ambayo hawaipati kwenye Vyuo ama kwenye Taaluma zao.
“Kitu cha kwanza ninachokifanya ni kumtuliza kijana ajue kwamba makosa ni sehemu ya maisha. Huwa nawafundisha na kupitia mimi wanasaidika” amesema Mwl. Joyce

Mwalimu Joyce anasema amekuwa akipokea kesi mbalimbali za Vijana hususani kwenye mahusiano ambapo unakuta Binti anakwambia anatamani kujiua au kuacha Shule, mwingine kutamani kuacha kazi kwa sababu ameumizwa na mpenzi wake.
“Mwingine anakwambia nilitamani kujiua, lakini nimemsaidia amekuwa sawa, pia huwa nafanya counselling kila saa mbili, mwingine anakwambia mpenzi wangu anataka kuniacha kwahiyo najaribu jinsi ya kumtoa kwenye hayo mawazo ili awe na malengo” anaeleza Mwalimu Kisha.

Katika mazungumzo hayo Mtangazaji wa Uhondo Media akafanikiwa kumuuliza swali kuwa je! Vijana ambao wanapenda uzinzi huwa unawasaidia vipi? Kwa sababu tumeona hiyo imekuwa ni changamoto kubwa ambapo vijana hushindwa kutulia kwenye Mahusiano waliyonayo.
Akijibu swali hilo anasema hiyo inatokana na mtindo wa maisha hususani kupitia Teknolojia ambapo mitandao ya kijamii imekuwa ikiwapelekea kuwa na fikra potofu
“Ukiniangalia kwenye Youtube nimetengeneza Video fupi inayoeleza kwamba unaweka nini kwenye kichwa chako, unalisha nini ubongo wako, kwahiyo.Mimi ninawaasa Vijana wajitahidi sana kulisha ubongo wao vitu vyenye mwanga kwa sababu ni watu ambao wana nguvu , changamoto wanapenda kuigiza kama vile wanavyoviona mitandaoni”

Pia marafiki na makundi yanayowazunguka vijana ndiyo yanapelekea wao kufanya uzinzi

Mwalimu huyu anaendelea kusema kuwa namna nyingine ya kuwasaidia ni kuwaombea kwa sababu wengine wameshabobea lakini Elimu ina nguvu
“Kijana ukimfundisha vizuri na madhara anayoyaona basi ataogopa na kuona kwamba uzinzi sio kitu kizuri”

Mwalimu Joyce amesema ana malengo ya kuendelea kufanya makongamano mbalimbali ambapo atashirikisha na Vijana wa mtaani na makundi mbalimbali na pia anatamani kujiunganisha na Taasisi mbalimbali za Kiserikali zinazowasimamia Vijana.

Kwa Upande wake Madam Sophia Samson Sanga ambaye ni Mtaalamu wa Afya ya Akili kutoka Chuo cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS) amesema katika Kongamano hilo amewafundisha Vijana kuwa Mafanikio katika maisha yao yanategemea Afya ya Akili.
Mfano uwezo wa kukabiliana na changamoto katika maisha ya kila siku na unapoelekea kwenye mafanikio kuna changamoto mbalimbali ambazo utakutana nazo na jinsi ya kukabiliana nazo ni kutegemea na afya yake ya akili ikoje.

“Sehemu ya pili ilikuwa inazungumza kuhusiana na uzalishaji, uwezo wa kuzalisha. Kwamba endapo Afya yake ya akili ipo vizuri basi anaweza akafika kwenye hiyo njia ya mafanikio kirahisi na akafanikiwa kama ambavyo amejiwekea malengo” ameeleza Mtaalamu huyo.

Jambo lingine ambalo amezungumza nao ni kuhusu uhusiano na jamii inayomzunguka mfano akiwa Shuleni, Kazini au kanisani au popote pale anakuwa na jamii na watu wanaomzunguka na jamii hiyo inaweza ikawa na mchango gani kwenye mafaniko ni pale atakapojua jinsi ya kuhusiana nao na jinsi ya kujiunganisha nao na kutambua nani awe nae na nani asiwe nae” ameeleza Madam Sophia.

Ametoa Wito kwa Vijana kuangalia Afya zao za akili kwa sababu ndizo ambazo zimebeba mafanikio yao.

Nao Vijana walioshiriki wameeleza kuyapokea vyema mafundisho hayo ambapo watakwenda kutumia kuwasaidia Vijana wengine.

Ili kupata mafundisho hayo unaweza kumtafuta Mwalimu Joyce Kisha kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Youtube, Instagram, Facebook, Tiktok kupitia Jina la Mwalimu Joyce Kisha.au mtafute kwa Simu namba 074509443

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *