WIZARA YA NISHATI YAOMBA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 1.8

0

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ameliomba Bunge likubali kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 yenye jumla ya shilingi Trilioni moja, Bilioni mia nane themanini na tatu, milioni mia saba hamsini na tisa kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na taasisi zake.

“Naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Nane Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba Hamsini na Tisa, Mia Nne Hamsini na Tano Elfu (Shilingi 1,883,759,455,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

i. Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Saba Tisini na Nne, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia Nane Thelathini na Mbili Elfu (Shilingi 1,794,866,832,000) sawa na asilimia 95.28 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Tano Thelathini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,536,020,274,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Nane, Milioni Mia Nane Arobaini na Sita, Mia Tano Hamsini na Nane Elfu (Shilingi 258,846,558,000) ni fedha za nje; na

ii. Shilingi Bilioni Themanini na Nane, Milioni Mia Nane Tisini na Mbili, Mia Sita Ishirini na Tatu Elfu (Shilingi 88,892,623,000) sawa na asilimia 4.72 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Ishirini na Nne, Mia Mbili na Moja Elfu (Shilingi 69,524,201,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Kumi na Tisa, Milioni Mia Tatu Sitini na Nane, Mia Nne Ishirini na Mbili Elfu (Shilingi 19,368,422,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *