AWESO AFANYA MAAMUZI MAGUMU KULINUSURU BWAWA LA NANJA

0


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefika Wilaya ya Monduli kunusuru Bwawa la Nanja ambalo ni Tegemeo la Vijiji 30 katika chanzo Maji pekee baada ya kumeguka kingo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.


Amesisitiza kwamba pamoja na ugumu wa kukarabati bwawa hilo wakati likiwa na maji maamuzi magumu yafanyike wataalamu wa Wizara ya Maji watumie utaalamu wao kulifanikisha hiko kwani hakuna namna nyingine.

Akizungumza na mamia wa wananchi wa Kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni Waziri wa maji maelekezo kwa Wataalamu wa Wizara kama ifuatavyo kwanza kutumia taaluma zao kuhakikisha Bwawa hilo linakarabatiwa kwa dharula haraka kuanzia kesho tarehe 19.04.2024 kudhibiti maji kuebdelea kupotea pili kufanya usanifu wa kina nyakati za kiangazi kusudi bwawa hilo liweze kukarabatiwa kwa uhakika zaidi.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Fred Lowassa amesema Bwawa hilo ndio tegemeo la wana Monduli kwenye matumizi ya maji kwa Binadamu, mifugo na wanyamapori hivyo anaiomba Serikali ione namna ya kukarabati bwawa hilo kwa dharura.

Aidha, Wakizungumza katika nyakati tofauti madiwani wa kata zinazoguswa na bwawa hilo wameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwafikia kwa haraka na kutafuta suluhu ya utatuzi ya changamoto hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *