KALABA HAJAFARIKI, TAARIFA MPYA YATOLEWA

0

Taarifa kumuhusu Mchezaji wa zamani wa klabu ya TP mazembe na timu ya taifa ya Zambia Rainford Kalaba aliyeripotiwa kufariki jioni hii , mchezaji huyo inaarifiwa kuwa bado yupo hai

Mazembe walikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kutoa taarifa ya kifo cha mchezaji huyo lakini hivi punde Mazembe hao hao wametoa taarifa kuwa mchezaji huyo hajafariki ila yupo kwenye uangalizi maalumu [ ICU

Idara ya uokoaji iliwapa taarifa Mazembe kuwa Kalaba amefariki na vyombo vya habari vikaripoti hivyo baada ya Kalaba kufikishwa hospitali madaktari walibaini bado yupo hai lakini hali yake ni mbaya sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *