AZANIA BANK WAIPAMBA BUNGE MARATHON

0

Viongozi na wafanyakazi wa Azania Bank wameshiriki Mbio za Bunge Marathon zilizofanyika leo 13 April, 2024 kuanzia Viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

Mbio hizo za kuanzia Km 21, Km 10 na Km 5 zimeongozwa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson ambapo wadau mbalimbali wakishiriki wakiwemo Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Azania Bank wamesema wataendelea kushiriki shughuli mbalimbali za michezo na kutoa mchango wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *