Klabu ya Young Africans iliyoko Ligi Kuu imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Taarifa iliyotolewa leo na TFF imesema uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo ambapo pamoja na masuala mengine, Young Africans haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa Mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

“Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi, kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *