MWAKINYO AMJIA JUU TWAHA KIDUKU MITANDAONI

0

Bondia Hassan Mwakinyo ametoa tathimini yake juu ya bondia Twaha Kiduku baada ya kushinda pambano lake kwa TKO kwenye mzunguko wa tano dhidi ya bondia Harpreet Sigh kutoka India akidai kuwa Kiduku anatafuta mabondia wakuja kuachia pambano .

“Najutia usingizi wangu yaani leo ( Jana) umeonyesha kuwa wewe hauna sifa, wala vigezo vya kuwa pro, nimekuwa kwenye boxing kwa takribani miaka 17 sasa hakuna ushindi wa namna ile , Kibenju nertwork mlundwa imekubeba sana kutafuta bondia wakuja kuachia na hii ndio salama yako .” Mwakinyo

“Kama sio ofa na jamaa angeamua kukaza angekuvua nguo tena ,kiwango chako ni kibovu sana siku hadi siku haukui ki – mchezo Simba na Yanga zinafuzu kila siku na zinabadilisha walimu wewe unapigwa kila siku lakini ni kama umefunga nae ndoa .”

“Listern ukitaka kujilinganisha sawa na mtu kwa ubora make sure baadhi ya vitu mnafanana au unakuwa zaidi yake .”

Ameandika bondia Hassan Mwakinyo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram baada ya bondia Twaha Kiduku kushinda kwa TKO dhidi ya bondia Herpreet Sigh kutoka India.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *