MBUNGE MAVUNDE AWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI KWA KUHIMIZA AMANI,UPENDO NA MSHIKAMANO
–Aitaka jamii kuwajali yatima,wajane na wenye ulemavu
–Atoa sadaka kwa vikundi vya yatima 11, wenye ulemavu na wajane 300
–Aahidi kuanzisha ujenzi wa msikiti kituo cha Watoto yatima Zam Zam
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza viongozi wa dini mkoani Dodoma kwa kuhamasisha umoja,upendo,amani na mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali itikadi za dini zao.
Mbunge Mavunde ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya kutoa sadaka kwa wajane,yatima na wenye ulemavu iliyofanyika katika Msikiti wa Gaddafi Jijini Dodoma ambao ni utaratibu wa kila mwaka wa Mbunge kukutana na makundi haya wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan
“Ninawapongeza viongozi wote wa Dini kwa kuendelea kuhubiri amani,umoja,upendo na mshikamano miongoni mwa watanzania.
Kupitia mahubiri yenu mmeifanya Tanzania imekuwa moja yennye mshikamano na umoja mkubwa.
Jamii ina wajibu wa kuwakumbuka na kuwajali watu wenye ulemavu,yatima na wajane ili kusaidia kutatua changamoto za makundi haya maalum”Alisema Mavunde
Akito salamu za shukrani,Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajabu Shaban amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuwajali yatima na wajane na akatumoa fursa hiyo kuwaomba waumini wa dini ya kiislamu kuwaombea viongozi wote wa Serikali wakiongozwa na Mh Rais Dkt. Samia S . Hassan ili wasimamie haki na kweli katika kuwaongoza watanzania.