BUNGE MARATHON KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI TATU KUJENGA SHULE.

0

Na: Emmanuel Charles

Zaidi ya Shilingi Bilioni 3 zinatarajiwa kukusanywa kupitia Bunge Marathon kwaajili ya kujenga Shule ya Wavulana pamoja na Viwanja vya Michezo vya Michezo kwaajili ya kuendeleza vipaji.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika 13 April Jijini Dodoma kuanzia katika viwanja vya Jamhuri ambapo watu mbalimbali watashiriki wakiwemo Wabunge wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani Dkt. Tulia Ackson.

Akielezea maandalizi Leo 09 April 2024 Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Bunge Marathon ambaye ni Mbunge wa Makete Mhe. Festo Sanga amesema zoezi la usajili linaendelea katika Vituo mbalimbali kwa kiasi cha Shilingi elfu 40 ambapo kupitia mbio hizo mshindi wa kwanza anatarajiwa kujikusanyia kitita cha Fedha za kitanzania Shilingi Milioni Tano.

“Marathon yetu ni mawazo ya mheshimiwa Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson na inafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu kutafuta fedha kwaajili ya kujenga shule ya wavulana ya Bunge Boys Sekondari, kwa sababu pia tumeshawekeza nguvu kwa wasichana katika sekta ya Elimu, tumeona pia kufuata maono ya Mheshimiwa Rais ya kuinua Elimu pia hata kwa mtoto wa kiume kwa kujenga Shule maalum kwaajili ya watoto wa kiume” Amesema Festo Sanga.

Kuhusu zoezi la Usajili Sanga amesema mpaka sasa Taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi zimeendelea kujisajili, pia wakimbiaji maarufu ambao wako nchini nao wameonesha ushirikiano na wanatarajiwa kushiriki.

Kuhusu zawadi ameeleza kuwa Mshindi wa kwanza atapata Kiasi cha Shilingi Milioni Tano

“Hii Marathon sio ya Bunge tu, ni ya watanzania wote, kuna zawadi ambazo tumeziandaa.na mshindi wa kwanza atapata Shilingi milioni tano kwa Km 21, pia kuna zawadi ya Mshindi wa pili na kuna zawadi ya Mshindi wa Tatu, kuna Km 10 tunaenda kutoa Milioni 3, lakini pia kuna Km 5, mkimbiaji anaenda kupata Milioni Moja na Laki Tano.” Ameeleza Mhe. Sanga

Mwenyekiti Sanga ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kupitia mataasisi na makampuni binafsi kuunga mkono juhudi hizo za kujenga Shule ikiwemo kutoa Vifaa vya Ujenzi ambapo pia amezishukuru baadhi ya Taasisi ambazo zimeshatoa Vifaa kama sehemu ya kusapoti.

Mbali na kuanza na kujenga Shule ya Wavulana pia maono ya Bunge Marathon ni kujenga Viwanja pamoja na Shule za Michezo.

Vituo vya Usajili vinapatikana katika Mikoa ya Dar es salaam na Dodoma ambapo kwa Dar es salaam ni katika Ofisi za Bunge, Mlimani City na Dodoma ni Shoppers Plaza, Jamhuri, Safina House pamoja na Bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *