MBUNGE KEISHA ATOA MITUNGI YA GESI KWA WATU WENYE ULEMAVU NA KUWAFUTURISHA.

0

Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Khadija Shaaban Taya (Keisha) amefanya Ibada ya Iftar kwa Makundi Maalum ikiwemo watu wenye ulemavu leo 07 April, 2024 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma.

Mbali na Iftar hiyo pia Mbunge Keisha ametoa mitungi 200 ya gesi kwa watu wenye Ulemavu pamoja na Makundi mengine ikiwa ni kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kwamba kila mtanzania anatumia nishati safi ya kupikia.

Mgeni Rasmi katika Shughuli hiyo alikuwa ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira, na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (Mb)

Akizungumza Mbunge Keisha amesema kilichofanyika ni mwendelezo wa kile ambacho amekuwa akikifanya katika kuwasapoti watu wenye Ulemavu na kusikiliza Changamoto zao na kuziwasilisha sehemu husika ikiwemo Bungeni.

Ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa mambo makubwa anayoendelea kuwafanyia watu wenye ulemavu nchini.
“Na Mimi ninapoendelea kusema pale Bungeni haina maana kwamba sifurahishwi na mambo ambayo yamefanywa ila jinsi ambavyo changamoto zinapozidi kutatuliwa ndivyo ambavyo changamoto zingine zinaendelea kuonekana, hatuna nia mbaya, nia yetu ni kujenga” amesema Keisha

Viongozi wengine waliohudhuria ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Zainabu Katimba

Mbunge Keisha Ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kurejesha asilimia mbili ambayo anaamini kuwa ni ukombozi kwa watu wenye ulemavu na wao wanatamani warudishiwe ili kujikwamua kimaisha na kiuchumi.

"Uzuri Naibu Waziri wa Tamisemi yupo hapa, naomba katika Halmashauri zetu Asilimia mbili peke yake zitawasaidia wajasiriamali, lakini kuna masuala ya mafuta ya watu wenye ualbino, kuna Vifaa kama (wheelchair)), fimbo za watu wasioona na kadhalika, tunaomba Ofisi yenu kupitia Halmashauri zenu ziendelee kutoa Vifaa ili maisha yetu yawe rahisi"

Katika hatua nyingine, Mhe. Keisha amewashukuru watu wote waliomuunga mkono akiwemo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde ambaye pia ni Waziri wa Madini.

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada mbalimbali katika kuwahudumia watu wenye ulemavu na wao kama Wizara wataendelea kufanya jitihada mbalimbali kuwazingatia watu wa Kundi hilo.

“tumefungua mfuko maalum kwaajili ya watu wenye ulemavu, Khadija Taya amefanya kazi hiyo na Fedha tayari tuna Shilingi Bilioni Moja kwaajili ya watu wenye Ulemavu”

Mhe. Katambi amempongeza Mbunge Keisha kwa Jambo hilo la kufuturisha alilolifanya ambalo sio dogo kwani ni kutokana na upendo mkubwa alionao kwa watu wake “
Alichokitoa hapa sio futari wala sio maji au soda, ametoa upendo wa dhati na moyo wa kujitoa tumekula upendo wake, tumekula matumaini yake, tumekula imani kubwa aliyonayo kwenu.tumlipe hiyo kwa kuendelea kumfanya kuwa Kiongozi wetu, Imani huzaa imani”

Amesisitiza kuwa Keisha amefanya mengi makubwa ambayo anastahili kuungwa mkono kwani sio wote wanaweza kufanya kama yeye kwani hata gharama alizozitumia angeweza kuamua hata aende kwa ndugu zake kutoa au hata kuamua kupanda ndege aende Dubai.

Kwa Upande wake mwakilishi wa Mufti amesisitiza Waislam wote kutoa kwa watu wenye hitaji kama alivyofanya Mbunge Keisha.

Mbali na Viongozi hao wa Serikali Ibada hiyo imehudhuriwa pia na Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *