SINA MPANGO WA KUONDOKA YANGA – AZIZ Ki

0

Kiungo wa Yanga SC, Aziz Ki amewaambia mashabiki wa Yanga kwamba hana mpango wa kuondoka Jangwani, kwani kilichomleta kwenye timu hiyo bado hajakifanikisha.

“Hata pesa hauwezi kufikia kiwango cha upendo nilio nao kwa klabu hii (Yanga),” ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram akisistiza kwamba kilichomleta ni kutwaa mataji ya kimataifa na bado hajafanikiwa.

Ki amesema hayo baada ya kuhusishwa na miamba ya soka ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns wanaodaiwa kutaka kumsajili.

“Nina deni kubwa kwenu (mashabiki wa Yanga) na Yanga ni familia yangu,” ameeleza zaidi baada ya shabiki mmoja kumuuliza kama ni kweli anaondoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *