WIZARA YA MAJI YATAMBUA MCHANGO WA SPIKA WA BUNGE KATIKA MAFANIKIO

0

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzua Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amepokea Tuzo maalum ya Siku ya Maji Duniani kutoka kwa Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso kwa kutambua mchango wake na Bunge kwa ujumla katika sekta hiyo tukio lililofanyika leo tarehe 5 April, 2024 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Tuzo hii awali ilitakiwa kutolewa Tar.22 Machi 2024 katika maadhimisho ya siku ya Maji Duniani ambapo Mhe Spika Dkt Tulia alikua nje ya nchi katika majukumu mengine.

Aidha, Tukio hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi. Kundo Andrea Mathew, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi. Mwajuma Waziri, Naibu Katibu Mkuu Bi.Agnes Meena pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amekabidhi Tuzo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Mhe. Jackson Kiswaga kwa niaba ya Kamati ikiwa ni sehemu pia ya kutambua mchango wa Kamati nzima katika Mafanikio ya Sekta ya Maji.

Tuzo hizo hutolewa tarehe 22 Machi maadhimisho ya siku ya Maji Duniani kila Mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *