TUENDELEE KUELIMISHA WAKULIMA JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI”

0

Haya yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Kemirembe Lwota alipokuwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani leo tar 04 April 2024 iliyofanyika kata ya Heka.

” Ninawaomba sana viongozi wa vyama hivi vya Ushirika pamoja na wataalamu wetu kuendelea kutoa elimu kwa wakulima wetu juu ya matumizi ya mfumo huu wa stakabadhi ghalani kwani ni kwa manufaa yao”

Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao serikali umeuanzisha ili mkulima apeleke mazao yake ghalani, lengo ni kuongeza thamani ya mazao na mkulima kupata bei inayoendana na jasho la uzalishaji. Alisisitiza Mhe. Kemirembe

“Wito wangu kwa wakulima ni kuhakikisha mnazingatia muongozo uliotolewa na serikali kuhusu mfumo huu na mfumo huu ni kwa manufaa yenu na utawasaidia kuboresha maisha yenu.”

Lakini pia wito wangu kwa vyama vya ushirika na viongozi ni kuhakikisha mnasimamia mfumo huu kwa ufanisi na kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati na mtatue malalamiko yoyote yanayojitokeza

Sambamba na hilo Mhe. Kemirembe ameendelea kusisitiza juu ya matumizi ya Mbolea kwenye Kilimo ili kuongeza uzalishaji.

“Ndugu zangu lazima tujue kuwa tunapaswa kuongeza uzalishaji katika kilimo chetu kwa kuhakikisha tunatumia mbolea ya kutosha wakati wa kulima”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *