GAMONDI AGOMA KUWATUMIA AKINA PACOME.

0

Kocha Mkuu wa Yanga Sc Muargentina Miguel Gamondi amesema katika Wachezaji wake watatu wenye majeraha kuna mmoja ndo anaweza kumtumia kwenye Mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika hapo kesho dhidi ya Mamelod Sundowns.

Gamondi ametoa kauli hiyo Jijini Pretoria kwenye Mkutano na Wanahabari leo 04 April 2024.

“Tunasubiri kuona itakavyokuwa leo kwenye mazoezi ya mwisho, tunaweza kumpata mchezaji katika wale waliokuwa majeruhi. Ni kweli tunaiwaza nusu fainali ya CAF lakini tunajali pia na usalama wa afya za wachezaji wetu pia. Young Africans haichezi mashindano haya peke yake” amesema Gamondi.

Wakati huo huo katika mazoezi ya Yanga Pacome Zouazoua ameonekana akifanya mazoezi ya peke ake huku Kocha Gamondi akimfuatilia kwa makini ili kuona kama ataweza kumtumia.

Wengine waliokuwa kwenye majeraha ni Khalid Aucho, Kouassi Yao na Kibwana Shomari ambao waliukosa mchezo wa awali.

Yanga itashuka dimbani hapo kesho 05 April 2024 kumenyana na Mamelod Sundowns katika Uwanja wa Loftus Majira ya Saa 3:00 Usiku kwa Saa za Afrika Mashariki.

Ikumbukwe katika mchezo wa awali uliochezwa uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam timu hizo zilitoshanga nguvu kwa suluhu ya 0 bin 0.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *