MAFUTA YAPANDA BEIPETROL TSH 3,257,DIZEL 3,210 DSM

0

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za Mafuta ya petroli zitakazotumika kuanzia leo Jumatano, 3 Aprili 2024.

Mabadiliko ya bei yamechangiwa na: kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) katika soko la dunia kwa wastani wa 3.94% kwa mafuta ya petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya dizeli, kupungua kwa gharama za kuagiza mafuta (premiums) kwa wastani wa 4.28% kwa mafuta ya petroli na kuongezeka kwa wastani wa 0.76% kwa mafuta ya dizeli kwa bandari ya DSM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *