BENKI YA AZANIA YADHAMINI HAFLA YA ‘FUTURU YA MAMA SAMIA’ SERENGETI

0

Benki ya Azania imedhamini hafla ya ‘Futuru na Mama Samia’ iliyoandaliwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Said Mtanda ambaye amehamishiwa mkoani Mwanza na kufanyika kwenye ukumbi wa Kisare mjini Mugumu, Serengeti Aprili 2, 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara.

Hafla hiyo pia iliambatana na kugawa misaada ya vyakula mbalimbali kwa makundi maalum, yakiwemo ya watu wasiojiweza, wenye ulemavu na watoto yatima wilayani Serengeti, Mara.


Viongozi mbalimbali waliohudhuria akiwamo sheikh wa Wilaya ya Serengeti,Juma Simba  waliishukuru benki ya Azania kwa udhamini ilioutoa kufanikisha tukio hilo kwani kufuturisha ni kujenga mahusiano baina ya binadamu, ni maagizo ya Mwenyezi Mungu kuwakumbuka na kufuturisha wasio na uwezo.
RC Mtanda pia alitumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa Mkoa wa Mara Kufuatia kuhamishiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza.

Kwa upande wa Benki ya Azania, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Dkt Rhimo Nyansaho alisema Benki ya Azania inatambua umuhimu wa kufunga, kufanya maombi na kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *