WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI KUNUFAIKA NA ADRA DODOMA

0

Zaidi ya Kaya 100 na watoto 190 wenye ulemavu wa ngozi wamenufaika na mradi wa AGRA AFRIKA uliohusisha watoto wenye ulemavu huo pamoja na kuwasaidia walezi wao kwa kuwapatia bima za afya na mahitaji mbalimbali ikiwemo mafutata ngozi ,miwani , na mahitaji ya shule ili kuwawezesha kutimiza malengo yao kikamilifu Hususani katika masomo .

Jackrine Raphael mama mwenye watoto watano ambao Kati Yao watatu Wana ulemavu wa ngozi amekuwa mwingoni mwa wanufaika wa mradi huu ambapo anasema Kabla ya kupewa msaada huo hali ilikuwa ngumu katika kuwatibia watoto hao.

“Yani kiukweli kuwalea watoto watatu wenye ulemavu ngozi NI kazi kwasababu unatumia Mda mwingi kuwaangalia ili wasidhurike na Mionzi ya jua na ukizingatia Mimi na mume wangu atuna kazi yakutuingizia kipato kikubwa mana tulikuwa na duka lakini kwasababu mahitaji yetu yanatoka hapo mtaji ulikuwa na kwenda kutafuta kazi mbali auwezi kwasababu watoto nani atawaangalia”alisema jack.

Mama Huyu anaendelea kusema amepitia unyanyapaa uliokuwa ukimuumiza kisaikorojia.

“Nilivyozaa mtoto wa Kwanza alikuwa mweupe kila Mtu alikuwa ananinyooshea vidole akipita Wanamuita Doli lakini utafanyaje ndo mtoto wangu lakini mtoto wa pili na watatu walikuwa weusi alivyogata wa nne na watano wakawa weupe tena kiukweli nilikuwa naumwa namba watu wanavyowaangalia watoto wangu ninachoshukuru Mme wangu hakunikataa.”

Anaendelea kusema” kuwa kuja Kwa msaada imewasaidia kwasababu huduma za matibabu na mahitaji mengine ambayo niya gharama si chini ya laki 6 sasa yatawezekana na watoto kwenda shule bila changamoto yoyote pia naomba mashirika na wadau wengine kuendeleza kutugusa”

Mratibu Msaidizi wa mradi AFRIKA Adra UPENDO KAJIRU Amesema walishirikiana na serikali za mitaa kutafuta Kaya duni ambazo zina watoto wenye ulemavu wa ngozi ili kuzisaidia Kaya hizo BIMA na mitaji ya kukuza uchumi wao na matunzo sahihi .

“Mradi huu unatekelezwa katika mkia WA morogoro na Dodoma malengo NI kufikia Kaya 400 Ila Kwa mkoa wa Dodoma teyari tumezifikia Kaya 190 ,pia tuliona pamoja elimu kuwa bure lakini mtoto mwenye ulemavu bado anamahitaji mengi kutokana na vifaa vyake vya kuzuia Mionzi ya jua ambayo NI kama laki sitaki na ukizingatia Kaya hizo NI duni kwaiyo tumewapa vifaa na mitaji ili waweze kuwalea vyema watoto hao na watimize malengo Yao

“Amesema kwakuwa mradi huo unaelekea mwishoni ameisisitiza jamii kuendeleza kutoa michango yao kupitia mfuko uliofunguliwa wa kuwasaidia watoto hao kupitia namba za simu.0749552658. Na nmb 51710075869
Educatin fund for children albnism jina la account kwa kiasi chochote utachoguswa .”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *