MWENYEKITI WA KIJIJI JELA MIAKA MINNE KWA KUPOKEA RUSHWA
Mahakama ya Wilaya Kiteto,
Imemhukumu MAMBE MOHAMED MAMBE, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nasetan, Kata ya Engusero, Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kuamriwa kwenda Jela miaka minne au kulipa faini ya shilingi 1,000,000/= kwa makosa ya kuomba na kupokea hongo kiasi cha shilingi 60,000/= kinyume na k/f 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.
Hukumu hiyo dhidi ya MAMBE MOHAMED MAMBE katika kesi ya jinai Na.20/2023, imetolewa na Mhe. Boniface Lihamwike, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Machi 27, 2024.
Mshtakiwa aliomba hongo ya sh. 60,000/= ili asimchukulie hatua za kisheria mwananchi ambaye alifanya mkutano wa wafugaji bila kibali cha serikali ya kijiji.
Mshtakiwa ameshindwa kulipa faini na amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.