DKT. TULIA AKUTANA NA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA INDONESIA

0

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Machi, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Puan Maharani katika Ofisi ndogo za IPU zilizopo katika Ukumbi wa CICG Geneva nchini Uswisi.

Katika kikao hicho, Viongozi hao wamejadili kuhusu namna bora ya kuendeleza mashirikiano baina ya Bunge la Indonesia na IPU pamoja na kuendeleza jitihada za kukuza mifumo ya kuinua wanawake kwenye mabunge duniani kote.

Mhe. Puan Maharani ni Balozi wa kuchagiza usawa wa kijinsia, nafasi ambayo anaitekeleza kwa ombi maalum la IPU.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *