KUIONA YANGA VS MAMELODI JUKWAA LA MZUNGUKO NI BURE

0

Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said pamoja na Kamati yake ya Utendaji wamekubaliana kuwa mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini siku ya Jumamosi ya March 30, 2024  itakuwa bure sehemu za mzunguko.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe akieleza kuwa wameamua hivyo kwa kuzingatia kuwa mechi inachezwa usiku saa 3:00 hivyo wanawapunguzia Mashabiki gharama.

Yanga wametangaza gharama zao za tiketi zitakuwa VIP A Tsh 30,000, VIP B Tsh 20,000 na VIP C Tsh 10,000.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *