WIZARA YA KILIMO IMEJIPANGA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA KAMATI YA BUNGE

0


Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde (Mb) amesema Wizara ya Kilimo itanyafanyia kazi maelekezo na maoni yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Kilimo, Mifugo na Uvuvi yaliyotolewa wakati kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Tasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Mlingano kilichopo wilayani Mheza Mkoani Tanga.

Naibu Silinde meyasema hayo baada ya kupokea maelekezo, maoni na ushauri wa kamati hiyo ilipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kujionea ukarabati wa majengo manne ya maabara pamoja na ujenzi wa maabara ya kisasa.

Aidha Mhe. Silinde amesema ukarabati wa miundombinu na ujenzi wa maabara mpya ya Tissue Culture utakamilika ifikapo mwezi Aprili 2024 . Mhe. Silinde ameahidi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za ukaguzi wa maendeleo ya mradi.
Naibu Waziri Silinde ameongeza kuwa Ukarabati huo umelenga kukipandisha hadhi kituo hicho na kuwa kituo cha umahili ( Centre of Excellence) ili kiweze kufanya utafiti wa udongo na mazao zaidi ya moja ikiwa ni pamoja na mazao ya vioungo na zao la nazi.

Kuhusu maabara ya TIssuu Culture amesema malengo yake ni kuongeza uzalishaji wa miche ya mkonge i kutoka miche milioni moja na laki tano kufikia miche milioni kumi kwa wakati mmoja. Lengo kuu likiwa ni kutekeleza maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuikuza sekta ya kilimo kwa asilimia 10 ifikapo Mwaka 2030.

Kwa upande wake Mwenyeki wa Kamati hiyo Mhe. Deo Mwanyika amesema Kamati ya Bunge imeridhishwa na kazi inayoendelea na kuihauri TARI kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo kwa muda uliopangwa.

Mhe Mwanyika ameongeza kuwa malengo ya kituo hicho yanaendana na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo amesisisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji huo ili kuepuka kupeleka sampuli za udongo nje ya nchi kwa ajili ya vipimo vya afya ya udongo wa Tanzania jamba ambalo amesema halina tija kwa mustakbali wa ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Dkt. Thomas Bwana, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha ujenzi na ukarabati wa maabara hizo kwani utawezesha upatikanaji wa ithibati itakayowezesha kituo hicho kufanya kazi ya upimaji wa udongo na kupata matokeo yatayotambulika kimataifa.

Mkurugenzi Dkt. Bwana amesema fedha kiasi cha Tsh. milioni 350 zimepelekwa ambapo kiasi cha Tsh. Milioni 196,777,000/= kwa ajili ya ukarabati na Tsh. Milioni 153,223,000/= ni kwa ajili ya ithibati na kiasi cha milioni 256,362,505 ni kwa ajili ya ujenzi wa Maabara ya Tissue Culture.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *