DC SHEKIMWERI AIPONGEZA DUWASA KWA KUITIKIA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA

0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweri ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa kuitikia maelekezo ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupanda miti Dodoma.

Ameseyasema hayo leo Machi 15, 2024 wakati wa zoezi la upandaji wa miti 300 katika eneo la tenki kubwa la lita milioni tatu katika Mradi wa Maji wa Nzuguni.

“Hotuba kuhusu umuhimu wa kutunza wa mazingira, umuhimu wa kupanda miti zimekuwa nyingi nadhani sasa hivi tujielekeze kwenye vitendo zaidi”. Amesema Alhaj Shekimweri

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amesema Mamlaka imekuwa ikipokea na kutekeleza maelekezo ya kupanda miti kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kufanya Dodoma kuwa ya kijani na kutunza vyanzo vya maji.

Amesema tayari miti 2000 imeshapandwa kwa mwaka 2022, na kuanzia mwaka jana Novemba hadi kufikia leo tutakuwa tumepanda miti 2000 kwa maeneo tofauti tofauti.

Miti iliyopandwa ni Chanzo cha Maji Mzakwe 250, Nzuguni tanki dogo kupitia mbio za Mwenge miti 150, Bahi 300, Kibaigwa 400, Chamwino 300 na Kongwa 300 na leo Nzuguni miti 300 ikiwa umuhimu wake ni kutunza vyanzo vya maji kuwa endelevu na stamilivu kwa mabadiliko ya tabia nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *