ZIARA YA AWESO UFARANSA YAFANIKISHA MIRADI YA MAJI MWANZA,MOROGORO AWAMU YA 2 NA ZIWA TANGANYIKA
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo tarehe 14 Machi 2024 amefija Makao Makuu ya Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD ambapo amekutana na kuwa na mazungumzo na Uongozi wa Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD ukiongozwa na Marie-Hélène Loison Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo Ufaransa AFD
Mazungumzo hayo yamejikita katika uwekezaji na utekelezaji wa awamu ya pili ya Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira Ziwa Victoria katika Jiji la Mwanza ambapo Waziri wa Maji ameeleza umuhimu wa upanuzi wa Mradi huu unakwenda kumaliza kabisa uhaba wa Maji katika jiji la Mwanza ambapo Uongozi wa AFD umeridhia jambo hili.
Ikumbukwe, awamu ya kwanza ya Mradi huu imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali, Benki ya Uwekezaji ya Ulaya na Shirika la Maendeleo la Ufaransa.
Aidha Waziri wa Maji kwa upande wa Morogoro imewasilisha ombi la nyongeza ya uwekezaji wa fedha zitakazowezesha kuongeza ujenzi wa Miundombinu ya usambazaji maji pamoja na Miundombinu ya ujenzi wa Majitaka ambapo SFD walitenga kiasi cha Euro Milion 70 kwaajili ya ujenzi wa Miundombinu ya majisafi pekee.
Aidha Wizara ya Maji imewasilisha rasmi kwa mara ya kwanza ombi la Fedha kwaajili ya Ujezni wa Miundombinu ya kutoa Maji Ziwa Tanganyika kuyepeleka mikoa ya Katavi na Rukwa
Naibu Mtendaji Mkuu wa AFD amesema kuwa ombi hili limepokelewa na kitafanyiwa kazi na kuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa sana.
Akihitimisha Mhe Aweso amesema Hatua hii ni mafanikio ya ajenda iliobebwa na Wizara ya Maji katika ziara ya kikazi nchini ufaransa na itapelekea kufanikisha upatikanaji wa Maji katika maeneo ambayo miradi ya ujenzi wa Miundombinu imekamilika na inaendelea.