KAMATI YA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII YAIELEKEZA SERIKALI KUHARAKISHA UKAMILISHAJI WA UJENZI WA JENGO LA KUMBI ZA KUFUNDISHIA LA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII BUHARE-MUSOMA

0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imetembelea na kukagua jenzi wa Jengo la kumbi za kufundishia katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare-Musoma, Mara leo Machi 14, 2024 na kuitaka Serikali kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa jengo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatma Hassan Toufiq amesema jengo hilo ambalo limechelewa kukamilika kwa sababu mbalimbali ikiwemo mvua linapaswa kukamilishwa mapema iwezekanavyo ili lianze kutumika kama ambavyo imekusudiwa.

“Mwezi wa tano ambao mmesema jengo litakamilika liwe limekamilika kweli na tutarudi tena hapa kuangalia kama limekamilika,” alisema Mhe. Toufiq.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis imeihakikishia Kamati hiyo kuwa serikali itahakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilishwa kama ambavyo Kamati imeelekeza.

Kamati ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ipo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na imeshafanya ukaguzi wa miradi katika Mikoa ya Tabora na Mara na kesho itakuwa Mkoani Mwanza kwa ajili ya kazi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *