KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII YAFANYA ZIARA RUANGWA

0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Malisili na Utalii leo tarehe 13 Machi, 2024 ilifanya ziara ya kukagua mradi wa Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi katika kijiji cha Namkatila kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi ikiwa ni ziara ya ukaguzi wa miradi kabla ya kuanza uchambuzi wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ndg. Lucy Kabyemera walipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Namkatila wakati Kamati hiyo ilipokwenda kukagua mradi wa upangaji mipango ya matumizi ya ardhi.

Pia Mhe. Mwenyekiti wa Kamati alimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Namkatila Ndg. Ally Said Daftari la Ardhi la Kijiji la Hati za Haki Milki katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namkatila walipata nafasi ya kushuhudia ugawaji huo wa hati miliki za kimila kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Serikali waliohudhuria wakati wa ziara ya Kamati hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *