RAIS SAMIA ANA NIA NJEMA KWA WANANCHI WAKE-RC SENYAMULE

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo amebaini kuchelewa kuanza kwa Mradi wa kituo cha afya cha Ihumwa kilichopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambacho kinajengwa na Mkandarasi mzawa.

Ziara hiyo imefanyika Leo Machi 12, 2024 ambapo mbali na kituo hicho cha afya cha Ihumwa pia amekagua mradi wa Barabara ya Kizota kwa kiwango cha lami iliyo chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS)

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan analeta miradi hii ili kupunguza changamoto kwa wananchi wake na hatutegemei kuona bado watu Mko nyuma kwani miradi hii inakuja kwetu nyie wakandarasa wazawa kwani Serikali inatenda haki kwa kila mtu.

“Sitegemei kuona uzembe wowote ukijitokeza kwenye miradi inayoletwa kwani wakandarasi wengi wapo kwenye hatua ya kwanza na nguvu kazi za vijana ni muhimu ili kukamilika kwa wakati kwa miradi inayoletwa na kuzitendea haki fedha zinazotolewa na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora” Amesema Senyamule.

Kituo cha afya cha Ihumwa kinajengwa kwa fedha za Seeikali kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 ambapo miradi inayotekelezwa ni ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la wazazi, Jengo la Mama na mtoto, Jengo la utawala, Maabara, Jengo la kipimo cha Xray, Jengo la kufulia, Vyoo vya nje na kibanda cha Mlinzi.

Pia amekagua mradi wa uchimbaji wa visima vya maji
katika eneo la Ihumwa ambao umetumia kiasi cha Fedha shilingi Bilioni 1.3, Ujenzi wa Barabara ya kizota kwa kiwango cha Lami urefu wa Km7 unaogharimu kiasi cha Shilingi 8.6 na ujenzi wa shule ya msingi katika eneo la Chilwana Ihumwa unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 ambayo itajenga Madarasa 16, Jengo la utawala, vyoo vya nje na uwanja wa mpira.

Kwa upande wake Meneja wa TANROADS Bi. Zuhura Amani, amesema kama wanufaika wakubwa na wasimamizi wa miradi hii watahakikisha inamalizika ikiwa na ubora unaotakiw na kukamilika kwa wakati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *