FCC YAZINDUA SIKU YA KUMLINDA MLAJI DUNIANI

0

Tume ya Ushindani (FCC) imezindua rasmi Maadhimisho ya Siku ya Kumlinda Mlaji Duniani ambayo imelenga kutoa elimu ya masuala mbalimbali kuhusu mtumiaji ikiwemo haki za usalama za mlaji, kuchagua, kupata taarifa ya bei, ujazo pamoja maligafi zilizotumika katika bidhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2024 Jijini  Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu  wa Tume ya Ushindani  (FCC) Bw. William Erio, amesema kuwa kilele za Maadhimisho Siku ya Mlaji Kitaifa itafanyika Machi 15, 2024 Jijini Dar es Salaam, kuku mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.

“Siku ya kilele cha Maadhimisho ya Kumlinda Mlaji Kitaifa kutakuwa na kongamano pamoja na mada mbalimbali zenye lengo la kujenga uwelewa mkubwa” amesema Bw. Erio

Bw. Erio ameeleza kuwa tangu Machi 8, 2024 walianza kuadhimisha siku ya Kumlinda mlaji kwa kutoa elimu kupitia  Ofisi za FCC zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma pamoja na Arusha.

“Machi 13, 2024 tutakuwa na kliniki na walaji katika ofisi za FCC Mko wa Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na  Mbeya kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto pamoja na kutoa mwelekeo wa namna bora ya kutatua changamoto hizo” amesema Bw. Erio.

Amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa kwa kushiriki kliniki  kwa ajili ya kupata elimu na majibu ya hoja katika maeneo mbalimbali ambayo wengependa kujua kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo.

Maadhimisho ya Siku ya Kumlinda Mlaji Duniani mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Matumizi ya akili memba yanayozingatia haki na uwajibikaji kwa mlaji”.

Uzinduzi wa siku ya kumlinda mlaji dunia ulianzishwa  mwaka 1980 na  Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo na kutengeneza kanuni za kumlinda mlaji.

Mwaka 1983 Umoja wa Mataifa walianza kuadhimisha siku ya kumlinda mlaji dunia ambayo inafanyika Machi 15 kila mwaka ambapo Tanzania walianza kuadhimisha rasmi mwaka 2009.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *