USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE  STAMICO WALETA MAFANIKIO KWENYE MIRADI YAKE

0

Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO ) wamefurahishwa na  ushirikishwaji unaofanywa ndani ya Shirika  hilo na  mafanikio katika miradi yake.

Hayo yamesemwa  na Mhandisi Mchenjuaji kutoka STAMICO Mha. Happy  Mbenyange  wakati wa sherehe  za Maadhimisho  ya siku ya wanawake Duniani ziliyofanyika machi 8, 2024, katika wilaya ya Kingamboni, Mkoani  Dar es Salaam.

Mha. Mbenyange  amesema wanawake wanauwezo wa kufanya kazi nyingi kwa wakati moja  na kwa umakini  mkubwa, jambo lililothibitika kupitia mradi  wa kuzalisha Nishati mbadala ya kupikia ya Rafiki Briquette

‘”Niipongeze sana Menejimenti ya STAMICO kwa kuwekeza kwa wanawake na kuwapa nafasi sawa na wanaume  katika kusimamia miradi, jambo ambalo linatupa hamasa sisi wanawake kusimamia kwa bidii, ili kuondoa dhana ya uduni wa mwanamke katika kufanya kazi kwa ufanisi”

Ametoa rai kwa wanaume nchini kuendelea kutoa fursa na kuwasaidia wanawake kufikia malengo na mafanikio katika kazi mbalimbali wanazofanya.

Amewasihi wanawake kujiamini, kujituma na kuonesha uwezo wao pindi wanapopata nafasi ya kutekeleza majukumu mbalimbali.

Aidha amewahamasisha watoto wakike kuchangamkia fursa za kitaaluma hususani katika nyanja za sayansi  ili waweze kuongeza ushindani katika kazi za kihandisi.

STAMICO imeshiriki katika sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu kupitia ofisi zake za Dodoma, Dar es Salaam na Kiwira yakiwa na kauli mbiu ya ‘Wekeza kwa Wanawake kuharakisha maendeleo ya Taifa na Jamii’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *