NDEJEMBI AWATAKA MAMENEJA WA TARURA KUFANYA TATHIMIN YA UHARIBIFU WA BARABARA

0

OR-TAMISEMI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amewaelekeza Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Nchi nzima kufanya tathimini ya uharibifu wa barabara zilizoathiriwa na mvua za El-Nino kama iliyofanyika wilayani Liwale mkoani Lindi ili kuweza kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi.

Mhe. Ndejembi ameyasema ni wajibu wa TARURA kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata huduma bora ikiwemo wanafunzi kwenda shule, huduma za afya na kwingineko na tathimini hiyo iwasilishwe makao makuu ya TARURA ili hatua za kutafuta fedha ziweze kuwasilishwa.

Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara ya ukaguzi wa miundombinu iliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyeesha katika wilaya ya liwale mapema leo.

“ Kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Mohamed Mchengerwa niwaelekeze mameneja wote wa TARURA kuhakikisha wanafanya tathimini kwenye maeneo yao na kuiwasilisha haraka makao makuu ya TARURA ili hatua zaidi za kutafuta fedha ziweze kufanyika,” Amesema Mhe Ndejembi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *