MIRADI YA MAJI KABUKU-HANDENI KUKAMILISHWA KWA WAKATI

0

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amewahakikishia wananchi wa Kabuku wilaya ya Handeni Mradi wa Maji Kabuku-Segera kukamilika kwa wakati.

Aweso amesema haya alipopata nafasi ya kutoa salamu za Wizara ya Maji kwa wananchi wa Kabuku katika ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Isidor Mpango akiwa amenza ziara ya kikazi leo tarehe 21 Feb 2024 Mkoa wa Tanga.

Akizungumza na wana Kabuku amewaeleza kuwa kwa eneo lao Mradi Mradi uliopo ni wa muda mrefu na kwasasa kutokana na ongezeko kubwa la watu hautoshelezi tena, Hivyo amewaeleza juu ya uwepo wa Mradi mkubwa unaondelea kujengwa kwasasa wa Kabuku-Segera wenye gharama ya Bil. 25 ambao utakamilika mwanzo wa January 2025 kwa Maelekezo ya Mhe Makamu wa Rais Dkt Philip Isidor Mpango aliyotoa leo Kabuku.
Mradi huu utakapokamilika utafikia Vijiji 15.

Aidha, Akisisitiza zaidi baada ya Maelekezo ya Mhe Makamu Wa Rais amemtaka na kumuelekeza Mkandarasi wa Mradi huo wa Kabuku-Segera kuongeza kasi katika Utekelezaji wake na kuwa atausimamia na kuufuatilia kwa ukaribu sana.

Katika hatua nyingine Aweso amewaeleza wana Kabuku juu ya mradi wa Maji wa Kihistoria ambao ni suluhu ya kudumu ambao ni Mradi mkubwa  wa Miji 28 wenye Gharama ya Bil.171 unaotarajiwa kukamilika December 2024.
Mradi huu ukikamilika utanufaisha mitaa yote 60 kwa Handeni na Vijiji zaidi ya 70 kwa Handeni Vijijini

Mwisho Waziri Aweso amewaeleza wana Handeni kuwa kwa Wilaya ya Handeni ipo Miradi mingine inayoendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali yenye jumla ya 8 ya kiasi cha Bilion 8 ikiwa ni pamoja na Mradi wa  Bwawa la Kwenkambala thamani ya Bil.2.5 asilimia 40,  Mradi wa Bwawa la Manga Bil.2.5, Mradi wa Kang’ata wa Mil.994 upo asilimia 98 na maji yanatoka na Mradi wa Maji Gole wa Mil.500 asilimia 40.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *