KUELEKEA MASIKA 2024: TMA YAPONGEZWA KWA USHIRIKIANO NA WADAU

0

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ameipongeza TMA kwa kuendelea kushirikisha sekta mbalimbali nchini katika shughuli za utoaji wa huduma za hali ya hewa.

Alibainisha hayo wakati akifungua rasmi Mmkutano wa 24 wa Wwadau wa Uutabiri wa msimu wa mvua za Masika (Machi hadi Mei), 2024 uliofanyika katika ukumbi wa PSSSF, Dodoma, Tarehe 19/2/2024.

“Tunapoelekea kutoa utabiri wa mvua za Masika 2024, lengo kuu la kukutana hapa ni kuwezesha matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa wote na kwa wakati, ninapenda kuipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa kuendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika shughuli zao za utoaji wa huduma za hali ya hewa ambazo ni pamoja na utabiri wa misimu ya mvua.

Ushirikiano huu ni mfano wa kuigwa na unafaa kuendelea hasa katika kipindi hiki ambapo dunia pamoja na nchi yetu inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa”. Alisema Mh.Jaji Bakari

“Tunapojiandaa kupokea taarifa ya utabiri wa Masika, Machi hadi Mei, 2024 ni muhimu sana kila mmoja wetu kuwa na jukumu la kufuatilia kwa karibu, kuelewa, kupanga na kukabiliana na hali ya hewa inayotarajiwa katika sekta yake”. Alisisitiza Jaji Mshibe Bakari.

Awali, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri TMA, Dkt. Hamza Kabelwa alisema “Mkutano huu ni mwuendelezo wa sehemu ya ushirikishwaji wadau hususan wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika kuandaa taarifa zinazolenga kuchochea matumizi sahihi ya huduma za hali ya hewa.

Katika mkutano huu tutakuwa na majadiliano ambayo ni muhimu katika kuendeleza na kuimarisha utoaji wa huduma za hali ya hewa na matumizi yake kwa jamii.

Mkutano huu ni muhimu sana kwa wadau wa hali ya hewa katika kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zao”.

Naye mwakilishi kutoka Sshirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme – WFP) Sasha Guyetsky, Mkuu wa Utafiti, Tathmini na Ufuatiliaji, WFP Tanzania, aliishukuru TMA kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa kwa WFP pamoja na wadau wengine nchini.

Aaidha, alieleza kuwa hivi karibuni TMA na WFP wamesaini ushirikiano wa miaka mitano wa kiutendaji ili kuweza kuimarisha utoaji huduma za hali ya hewa wenye kuleta tija.

Mmoja wa wadau kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Consolata Mbanga alieleza namna taarifa za awali za msimu wa mvua za Vuli, 2023 zilivyosaidia katika kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo pamoja na kuandaa Mmpango Taifa wa Ddharura kwa mikoa iliyotarajiwa kuathirika kutokana na hali ya El Niño.

Katika mkutano huu, wadau walipata fursa ya kuona utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei, 2024 na kutoa michango yao juu ya athari zinazotarajiwa katika sekta husika pamoja na ushauri ili kuwezesha kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *