TUNAENDELEA KUSAPOTI JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUPITIA FILAMU YA THE ROYAL TOUR

0

Mhifadhi Mkuu,Msimamizi na Mratibu wa Masuala ya Mipango na Utalii Kanda ya kusini Jonathan Kaihura Amesema kuwa wao kama Hifadhi wanaendelea kusapoti juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya The Royal Tour kuwakaribisha watanzania kutembelea Hifadhi ya taifa kitulo.

Amesema kuwa pia wanaendelea kutangaza vivutio vilivyopo kupitia mkutano ,matamasha ,kuhakikisha kwamba watanzania wanatembelea maeneo hayo hasa ya Kanda kusini ikiwemo Hifadhi ya kitulo lakini pia wanatambaza nje ya nchi katika masoko mbalimbali kama urithi wa dhamani.

Kaihura ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa Habari ambao walitembelea Hifadhi ya kitulo Kwa lengo la kutangaza vivutio vilivyopo kwenye Hifadhi hiyo.

Akizungumza mikakati waliyonayo hususani kuvutia zaidi watalii Kaihura Amesema kuwa Katika eneo hilo Kuna utalii wa kutembelea kwasababu maeneo ni rafiki na hakuna wanyama wakutisha ,ambapo wanaweza kupanda baskeli ,pia wanafanya maandalizi ya kuongeza mazao mengine ya utalii na lengo ni kujalibu kuongeza mazao hayo.

Amesema.kwa upande wa Hifadhi ya kitulo wamefikia pazuri sana na wameshafikia hatua ya kupata farasi ili kuongeza mazao ya utalii na ili kuhakikisha Ikolojia Iko sawa wanaendelea kuongeza mistu ya asili Kwa kutumia watalaamu ambao Kila siku wanahakikusha kwamba maeneo hayo yanaendelea kubaki salama.

Mhifadhi Kaihura Amesema pia wanalenga kurudishia wanyama ambao wametoroka na hasa wanyama walikuwa wametoroka na wanaendelea kuwarudisha wanyama kama Zebra ,Pundamilia ,Swala.

Akizungumzia ushirikiano na jamii Kaihura Amesema wanahusika kutoa elimu Kwa jamaa hasa wanaozunguka maeneo ya Hifadhi ili kuhakikisha vyanzo vya Maji vinalindwa kwasababu eneo hilo lipo juu na ndio chanzo kikubwa cha Maji yanayotirirka maeneo ya Ihefu, Usangu ,Mpaka Mto mkubwa wa Ruaha kwahiyo maeneo hayo lazima elimu itolewe ya kutosha.

Amesema kwasababu uhifadhi ukiwa mzuri hata wananchi wanaozunguka maneo hayo wanafaidi na wameshatoa mizinga 185 Kwaajili ya kusaidia wanakijiji kusudi waweze kujua umuhimu wa uhifadhi lakini kama shirika ili kurudisha Kwa wananchi wametoa pesa Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya hospitali ,nyumba ya mganga mkuu , madarasa , katika Vijiji vinavyozunguka Hifadhi na nyumba  za walimu hayo yote yanatokana na kile wanachokipata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *