MILIONI 700 KUJENGA OPD KITUO CHA AFYA LIKOMBE

0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Mhe Dkt Festo Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali kupitia mapato ya ndani, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara itatenga Sh Milioni 70 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha Afya Likombe mkoani Mtwara.

Mhe Dkt Dugange ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Tunza Malapo aliyehoji ni lini Serikali itakarabati jengo la ‘OPD’ na kujenga uzio katika kituo cha afya Likombe-Mtwara Mikindani.

Amesema Kituo cha Afya Likombe ni moja ya vituo vya afya vilivyonufaika na mpango wa maboresho ambapo katika mwaka wa fedha 2017/18 kituo hicho kilipokea Sh Milioni 500 na kujenga jengo la wazazi, maabara, jengo la kuhifadhia maiti, stoo ya dawa, nyumba ya mtumishi na kichomea taka.

“ Pamoja na maboresho makubwa yaliyofanywa katika kituo hicho bado kuna uhitaji wa jengo la kuhudumia wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na uzio.

Katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali kupitia mapato ya ndani, Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara itatenga Sh Milioni 70 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha Afya Likombe,” Amesema Mhe Dkt Dugange.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *