WATUMISHI GST WAPATA ELIMU YA ZIMAMOTO

0

Watumishi wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wamepata fursa ya kupatiwa  mafunzo ya kujikinga na majanga ya moto pindi yanapotokea kutoka kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania.

Mafunzo hayo yametolewa leo Februari 08, 2024 na Jeshi hilo yaliyofanyika katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma uliopo katika ofisi za taasisi hiyo jijini Dodoma.

Akitoa maelezo kwa watumishi wa taasisi hiyo, Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mary Messo, ameeleza namna mbalimbali za kupambana na moto pindi unapotokea kwa kutumia vifaa vya Zimamoto (Fire extinguisher) ikiwemo mitungi, Zulia maalumu na nk.

Aidha, Koplo Messo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa watanzania kutumia namba ya dharula ya Zimamoto na Uokoaji ambayo ni 114 kutoa taarifa ya moto ili usaidizi kufika kwa wakati.

Akijubu swali la Mjiolojia kutoka GST Khamis Said Kuhusu tatizo la Maji katika magari ya kuzimia moto kuwa machache, Messo amesema kuwa, Kila wakati huwa wanabeba maji ya kutosha lakini kinachotokea ni kwamba tenki moja la maji  huweza kuisha ndani ya dadika 3 hadi 15 kutokana na kasi ya maji yanavyotoka na hivyo kuisha haraka wakati mwingine kabla ya moto haujazimika.

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Utawala na  Uendeshaji Bi. Neema Mhagama amefungua mafunzo hayo kwa watumishi wa GST yenye lengo la kupata elimu  ya  namna ya kukabiliana na changamoto za ajali za moto  mahali pa kazi na mazingira mengine yanayowazunguka.

Pamoja na mambo mengine, Mhagama amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kazi nzuri wanayoifanya na pia, amelipongeza Jeshi hilo kwa kutoa elimu hiyo kwa watumishi wa taasisi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *