MRADI WA DMDP KUUNGANISHA WILAYA ZA TEMEKE NA MKURANGA
Katika jitihada za kuendelea kuwaunganisha Wananchi wa Wilaya mbili za Temeke na Mkuranga, Serikali imepanga kuboresha kwa kujenga madaraja/makalavati ya Churwi, Tabowa na Majimatitu kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbagala, Mhe Abdallah Chaurembo aliyehoji mpango wa Serikali katika kuziunganisha Mbagala na Mkuranga..
“ Malengo ya Serikali ni kuziunganisha Wilaya za Temeke na Mkurang, mpaka sasa maeneo matatu ya Kilwa, Tambani na Rufu Nampombo yameunganishwa kwa madaraja/makalavati na yanapitika kwa mwaka mzima. Kwa sasa serikali imepanga kuboresha kwa kujenga madaraja/makalavati ya Churwi, Tabowa na Majimatitu kupitia mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP).