TIMU YA EWURA YAFIKA MASWA KUTATHMINI BEI YA MAJI
Timu ya watalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji nchini, (Ewura) imefika katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu kufuatilia na kufanya tathmini ya kina juu bili za maji.
Wataalamu hao wamewasili leo Januari 30, 2024 kufanyia kazi malalamiko ya wananchi wa Maswa waliyoyatoa kwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda wakidai kwa Mamlaka ya Maji ya Maswa inawatoza bili kubwa ya maji.
Baada ya malalamiko hayo yaliyotolewa jana, Makonda aliwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ambaye alitoa ahadi kwamba ndani ya siku moja angewaelekeza mamlaka husika (Ewura) kufika na kufanya tathmini upya na kuja na ushauri juu ya kiwango sahihi cha wananchi kuchangia huduma hiyo.