BRELA YAWAASA WAFANYABIASHARA KWENDA KUPATA ELIMU YA KUJISAJILI KUPITIA MFUMO WA MTANDAO.

0

Na; Emmanuel Charles-Dodoma

Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni Brela imesema kupitia zoezi la kusajili huduma kupitia mtandao limesaidia kupunguza gharama na kusababisha mtu kusafiri umbali mrefu kupata huduma ikiwemo kusajili kampuni au Biashara.

Akizungumza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma Winfrida Gaudence ambaye ni Afisa Leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) amesema wateja wanaofika katika banda la Brela wanapata Elimu juu ya kutumia mfumo huo wa Mtandao ili kujipatia huduma wanazohitaji.

“Kutokana na kwamba saivi huduma zetu ziko kwenye mfumo hii imesaidia sana wateja kupata huduma akiwa popote pale alipo hata akiwa nyumbani anaweza akaingia kwenye mfumo na akafanya maombi yake kwenye mfumo na akapata cheti chake hapo hapo, inawapunguzia hata zile gharama ambazo zamani mtu alikuwa anatoka mbali mfano Kigoma hadi Dar es salaaam ili aweze kuhudumiwa” Ameeleza Winfrida.

Aidha, Winfrida ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia wiki hiyo ya sheria kufika kujisajili kwa urahisi na haraka pamoja na kupata Elimu ya masuala mbalimbali kuhusu huduma za Brela.

“Wafanyabiashara watumie wiki hii ya Sheria kama fursa ya kuja kutatua changamoto mbalimbali na kujisajili majina yao ya biashara kwa sababu tunatoa huduma hizo hapa hapa na mteja akija anapata cheti chake cha usajili”.

Pia Afisa Winfrida amesema tangu kuwepo kwa wiki ya Sheria kumekuwa na mwitikio mkubwa ikiwemo watu kufika kujisajili na kupata Elimu.

Pamoja na hayo bado watu wana changamoto ya kushindwa kuutumia Mfumo huo wa Brela lakini Wakala amekuwa akijitahidi kutoa Elimu ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *