SAMUEL ETOO ATOA DARASA LA UZALENDO KWA VIJANA WA AFRIKA
Samuel Eto’o kwa wachezaji wa Kameruni baada ya kufungwa na Senegal:
“Ndugu Cameroon imenifundisha kuwa ni askari ndani ya timu ya Taifa. Nitakufa na roho hii.Cameroon imetolewa kwa fedheha kwa sababu upendo kwa nchi hauko 100%.
Ningeweza kucheza mechi mbili siku moja kwa upendo wa nchi yangu. Nilifanya hivyo, Roger Milla alifanya hivyo, na François Omam Biyick alifanya hivyo.Je, mnafikiri Cameroon ilitulipa zaidi kuliko vilabu vyetu?
Mnacheza na wachezaji wengi wa akiba, mnachoogopa ni nini?Kufa kwa ajili ya nchi yako ni vyema kuliko pesa zote duniani.
Manga Onguené alivunja mguu wake kwa ajili ya nchi yake.Baada ya AFCON, mambo yatabadilika, tutakua na kipimo cha uzalendo kabla ya kuitwa timu ya Taifa.
NB: Watanzania tujifunze jambo hapa, kulipigania taifa kunahitaji uzalendo wa hali ya juu.