MWANASHERIA WA YANGA AISHAURI MAZITO SERIKALI NA TFF MBINU ZA KUWA NA TIMU BORA YA TAIFA YA MPIRA

0

Anaandikia @simon.esqHongereni sana @taifastars_ , binafsi siwadai, matokeo haya ndio kipimo chetu cha uwekezaji wetu kwenye soka.

Kwa maslahi mapana ya Taifa, nipende kushauri yafuatayo;

1. Tuziunganishe TFF & ZFF na tuwe na ligi moja bora yenye timu kutoka bara na Zanzibar.

2. Serikali itoe ruzuku kwa timu za vijana kama inavyofanya kwa vyama vya siasa.

3. Serikali ifute kodi na michango isiyo na tija kwa timu za mpira mfano NSSF, WCF, SDL, etc haina tija kwa wachezaji bali huongeza mzigo kwa vilabu, ianzishe kodi maalam ya zuio (WHT) kwa ajili ya wachezaji.

4. Hela zetu za FIFA za maendeleo ya mpira wa miguu zielekezwe kwenye kurekebisha miundombinu ya viwanja hasahasa sehemu ya kuchezea (pitch) ili ligi iwe na ubora zaidi.

5. TFF ianzishe mashindano ya vijana ya kitaifa nje na vilabu na yafanyike kila mwaka sambamba na kurudisha mashindano ya mashuleni.

6. Serikali irasmishe hadhi maalum za wachezaji wote wanaocheza nje ya mipaka ya Tanzania na wenye asili ya kitanzania watakaotaka kuja kulitumikia taifa.

7. Tulete wakufunzi na wataalamu wa soka la vijana, wapewe jukumu la kukuza talent kila mwaka, na vijana hawa wakulie sehemu moja.

8. Wadhamini wote wa michezo wapewe msamaha maalum wa kodi kwenye biashara zao, hii itavutia uwekezaji zaidi kwenye mpira wetu.

9. Serikali ianzishe scholarship maalum kwa wanafunzi wote wenye vipaji na kuwataftia akademi nje.

10. Kwakuwa AFCON ya 2027 tunaandaa wenyewe hivo hatutakua na presha ya kufudhu, tuandae timu ya taifa kuanzia leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *